Chanjo
itakayo wakinga watoto wa chini ya umli wa miaka mitano na virusi
vinavyosababisha kuhara (rotavirus) imezinduliwa nchini Uganda kwa
ushirikiano wa serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto UNICEF.

hiyo iliyozinduliwa rasmi Jumatatu katika wilaya ya Buikwe, itatolewa
bure kwenye vituo vyote vya afya nchini Uganda na inatarajiwa kuokoa
maisha ya maefu ya watoto wanaofariki Dunia kila mwaka kutokana na
ugonjwa wa kuhara.
Mwakilishi wa UNICEF, nchini Uganda Dokta Doreen Mulenga, ameipongeza
seriali ya Uganda kwa kujumisha chanjo ya rotavirus katika mpango wa
chango wa kitaifa na kusema ni hatua muafaka katika juhudi za kutimiza
lengo la afya bora kwa watoto wote, Taarifa hii nikwamjibu wa Radio ya Umoja wa Mataifa UN RADIO.