Unaposaidia
kuendeleza kipaji cha mwanao faida zake si kwake peke yake bali pia kwa
jamii nzima. Huo ndio wito uliojitokeza katika warsha ya siku tatu
iliyokutanisha wazazi, walimu na wanafunzi mkoani Pwani nchini Tanzania
kwa lengo la kutambua, kuendeleza na kufaidi na vipaji vya watoto
hususani yatima na wasiojiweza.
yatima au wanaoishi katika mazingira ya umasikini nchini Tanzania mara
nyingi hukosa fursa za maendeleo kielimu hata kimaisha kwa sababu ya
kutokuwa na ujuzi wowote limesema shirika lisilo la kiserikali la
COMPASSION ambalo ni la kidini linalowasaidia watoto na vijana yatima
katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s.
Shirika hilo linashirikiana na shule mbalimbali za mkoa wa Pwanni
hasa zinazotoa elimu kwa watoto yatima na masikini wasiojiweza kupata
ujuzi wa kuweza kujitegemea hapo baadaye.
Leo limekamilisha warsha ya siku tatu iliyokutanisha washiriki zaidi
ya 300 , walimu na wanafunzi kujadili jinsi ya kutambua, kuendeleza na
kufaidika na vipaji walivyonavyo lakini pia kuichagiza jamii kusaidia
kuendeleza vipaji vya watoto wao kwa ajili ya mustakhbali wao.
Mwanafunzi Rehema Egidi ni miongoni mwa washiriki
yatima na watoto kutoka familia masikini wakihudhuria warsha ya siku
tatu mjini Kibaha mkoani Pwani nchini tanzania, ya kjinsi gani ya
kubaini , kuendeleza na kufaidika na vipaji vya watoto hawa katika shule
mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya SDG’s
(REHEMA EGIDI)
Peter George ni mwalimu wa kazi za mikono
(SAUTI YA PETER GEORGE)
Baada ya siku tatu za warsh watoto wameambulia nini? Sarafina Alex ni mwanafunzi
(SAUTI YA SARAFINA ALEX)