ya mji wa Aden, nchini Yemen, msafara wa magari ukiwa na ugeni kutoka
UNICEF akiwemo Mkugurenzi Mtendaji Bi. Henrietta H. Fore.
Mwelekeo ni kituo cha afya cha Alqatee’a ambako analakiwa na wauguzi
na mama ambao watoto wao wamelazwa kupata huduma kutokana na magonjwa
yanayokabili watoto wao ikiwemo utapiamlo uliokithiri.
Watoto hawa ni miongoni mwa watoto milioni 11 nchini Yemen ambao
wanahitaji chakula, tiba, elimu , maji na huduma za kujisafi ambapo Bi.
Fore amesema..
“Tumekutana na akina mama kadhaa wakiwa na watoto wao,
wengi wao ni wachanga, na mama hao wanahitaji msaada mbalimbali, kabla
na baada ya kujifungua, ikiwemo lishe na malezi kwa watoto wao
nyumbani.”
Ametembelea pia kituo cha watoto kinachofadhiliwa na UNICEF ambako
watoto wanajifunza ikiwemo kuchora kama njia mojawapo ya kujieleza, na
ndipo akaelezea moja ya mchoro aliopatiwa.
“Anaonyesha dunia ambayo angependa awepo. Kuna basi
limebeba abiria, kuna lori na pia taa za barabarani ambazo hazipo Aden,
ameziona tu kwenye vitabu.Hapa anaonekana amependeza na rafiki yake wameketi. Kuna jua linawaka na nyumba anayopenda.”
Kwa mantiki hiyo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa, Umoja wa Mataifa
kuongeza usaidizi wao kwa Yemen ili watoto hao waweze kutimiza ndoto
zao baada ya machungu waliyopitia na kushuhudia nchini mwao Taarifa hii nikwa mjibu wa Radio ya Umoja Mataifa UN.