Burundi ya kuwapiga marufuku wasichana wajawazito na wavulana waliowapa
ujauzito huo kurudi shuleni, yakisema hatua hiyo ni ukiukaji dhidi wa
haki za elimu kwa watoto.
Mashirika hayo pia yanasema kuwa hatua hiyo ni ubaguzi dhidi ya mtoto
wa kike. Juma lililopita serikali ya Burundi ilitoa agizo kwa serikali
za mikoa ikisema kuwa wasichana wajawazito pamoja na wavulana
waliosababisha ujaouzito huo hawana haki ya kuwa sehemu ya mfumo wa
elimu nchini humo.
Katika barua ilioandikwa Juni 26 kwa
wakurugenzi wote wa elimu mikoani, waziri wa elimu Janvière Ndirahisha
alisema hata hivyo kuwa wanafunzi hao wataruhusiwa kuhudhuria mafunzo ya
kiufundi na kozi za kitaaluma.
Agizo ni la ubaguzi
Lakini
makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa kuwazuia watoto
kuhudhuria masomo kutakuwa na athari mbaya kwa elimu yao kwenye taifa
ambalo asilimia 11 ya wasichana kati ya umri wa miaka 15-19
wanajihusisha na vitendo vya ngono. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu.
Marufuku
hiyo ya taifa hilo la Afrika Mashariki, inalenga kuwazuia wasichana
zaidi ya watoto wa kiume, wanasema wanaharakati wakiongoza kuwa ni
rahisi kugundua kuwa mtoto wa kike ni mja mzito, lakini ni vigumu
kutambua aliyempa mimba.
Wakili wa kikundi kinachopigana dhidi ya
marufuku hiyo Naitore Nyamu-Mathenge, anasema marufuku hiyo inamnyima
mtoto wa kike elimu pamoja na kuegemea zaidi upande wake.
Anauliza,
“serikali inapanga kuthibitisha vipi kuwa mvulana fulani ndiye msichana
fulani mimba, na je itakuaje kwa visa ambavyo walimu na watu wazima
katika jamii wamehusika, je serikali itawachukulia hatua pia?”
Nilikuwa nahitaji kufanya kazi na poja na ninyi jinsi zaidi ya kupambambana na ubakaji wa watoto nchin
tanzania
Karibu sana Frida. Ntafurahi kuwasiliana na mimi tumia pia whatasApp no. +255767085647/ Email:[email protected]