Nchi nyingi duniani hususan zile za kipato cha chini bado zinaona si mtaji
kumpeleka shule mtoto wa kike, jambo ambalo hii leo Benki ya Dunia inasema
limepitwa na wakati, kwa kuwa ukiwekeza kwa mtoto wa kike umewekeza kwa dunia
nzima.
Fursa finyu za elimu kwa watoto wa
kike pamoja na vikwazo vya kumaliza miaka 12 ya elimu husababisha nchi husika
kupoteza kati ya a dola trilioni 15 hadi trilioni 30 ambazo zingalichangiwa na watoto
hao kupitia nguvu kazi katika jamii zao,Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya
Benki ya Dunia iliyotolewa kuelekea siku ya Malala mapema wiki hii.
Ikipatiwa jina la Fursa zilizopotezwa- Gharama ya kutompeleka shule mtoto wa
Kike, ripoti hiyo inasema hali ni mbaya zaidi kwa nchi za kipato cha chini
ambako watoto wa kike wanaohudhuria shule ni chini ya theluthi mbili.
Hatahivyo Riport hiyo imebainisha kwamba, wanaojiunga na shule ya sekondari
ya awali ni mmoja tu kati ya watatu ambaye anahitimu masomo hayo Taarifa hii
nikwamjibu wa Radio Wshirika UN RADIO.