Mabaraza ya
Watoto nchini yamehimizwa kutumia elimu wanayoipata kuibua vitendo vya ukatili
wanavyofanyiwa watoto ili kuondokana na vitendo hivyo. Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine
Ndugulile wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza
alipowatembelea na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.

Dkt.Ndugulile
amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 takribani wanawake na watoto 41,000
walifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kati yao 13,000 wakiwa ni watoto
pekee. Ameongeza kuwa vitendo vya ukatili vimeongezeka ukilinganisha na matukio
ya vitendo vya ujambazi nchini ambapo suala hilo halitakiwi kufumbiwa macho na
wananchi na wadau.

Aidha Dkt.
Ndugulile ametoa rai kwa wananchi hasa wazazi na watoto kutomalizana nyumbani
endapo vitatokea vitendo vya ukatili katika familia zao bali kuviripoti katika
mamlaka husika. Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Bw. Joel Festo ameishukuru Serikali na wadau kawa kuendelea kuwajali
watoto kuanzia katika utoaji wa huduma za afya na kutekeleza upatikanaji wa
haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa
na kutobaguliwa.

Dkt Ndugulile pia ametembelea na kujionea shughuli
zinazotolewa na Kituo cha utoaji Huduma za pamoja kwa wahanga wa ukatili wa
kijinsia (One Stop Centre) hapo mkoani Mwanza. Kwa upande wake Kaimu Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure Dkt. Bahati Peter Msaki amesema
kuwa Kituo cha utoaji Huduma kwa wahanga wa ukatili (One Stop Centre) kimekuwa
msaada mkubwa kwa wanajamii kwani wahanga wengi wa vitendo vya ukatili wamekuwa
wakipata huduma kutoka katika kituo hicho.