ya elimu Tanzania inaadhimisha juma hili ikibeba kauli mbiu
“uwajibikaji wa pamoja katika kutoa elimu bora, watoto wetu tunu yetu”,
madhumini ni kuchagiza ufikiaji wa lengo namba 4 la maendeleo endelevu
SDG’s lihusulo elimu.
Maadhimisho
haya ya wiki ya elimu yaliyoanza Julai 16 na yatakamilika Julai 20 na
yanafanyika nchi nzima yakishirikisha pia wadau mbalimbali wa elimu
yakiwemo mashirika ya kitaifa na kimataifa yanayosaidia kusongesha
ajenda ya elimu kama shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
UNICEF na shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.
Mkoani Morogoro Mashariki mwa nchi hiyo John Kabambala kutoka Radio
washirika Tanzaniakids FM ametembelea maonyesho ya wiki ya elimu ya
mradi wa elimu ya awali unaoendeshwa na shirika la Childhood Development
(CDO) kwa msaada shirika la Children in the cross Fire kutoka Ireland.
Mradi huo ni wa elimu kwa njia ya michezo kwa kutumia vitu vya asili
kama mawe, visoda, chupa na vitabu vya picha na unashirikisha shule
zaidi ya 40 mkoani humo na Kabambala amemuuliza afisa mradi Joseph
Machira kwa nini wameanzisha mradi huo nae amesema kwasababu kuna changamoto kubwa kwenye darasa la awali .
Integrated school readiness program ISRP in Swahili Watoto Wetu Tunu Yetu ni mradi unaolenga kuweka utayari wa mtoto kaingia darasa la kwanza mradi unalenga sana watoto kuanzia miaka 0-6 hasa wale walio darasa la awali, mradi unakenga kuboresha mbinu za ufundishaji wa darasa la awali kupitia michezo, mradi unasisitiza utumiaji wa zana za asili mfano chupa za Maji, magunzi, vizibo,visoda n.k pia tunasisitiza madarasa changamshi kwa darasa la awali pamoja na lishe mashuleni…Kwa pamoja tutayaboresha madarasa yetu ya awali
Asante sana nashukuru kwa ufafanuzi huo.
Uboreshaji wa Elimu ya awali ni kichocheo kikubwa sana katika ukuaji na Maendeleo ya watoto kwa kujenga utayari wao. Ushirikiano wa pamoja utajenga msingi wa watoto wetu. Karibuni sana tujifunze Elimu ya awali na manufaa yake kwenye Mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu Wilaya ya Mvomero kata za Mtibwa,Doma na Malali kwenye shule za msingi za Serikali zote pia Wilaya ya Kilombero Kata za Mwaya,Mchommbe na Ching'anda. Wekeza sasa kwenye elimu ya awali ya malezi makuzi na mendeleo ya watoto.
Shukrani sana Mr. Peter kwa ujumbe huo mzuri na kwamaoni yako karibu sana.