Makete Paralegal Oganization(MAPAO) lililopo mkoa NJOMBE ni Shirika la Wasaidizi wa kisheria lisilo la kiserikali linalo toa huduma ya Elimu na Msaada wa kiseria kwa jamii limetoa ufafanuzi wa kazi zake zinazofanywa nashirika hilo katika wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe kwa ujumla.
Katika kijiji cha KISINGA shirika hilo lilitoa Elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi KISINGA na kuwafahamisha juu ya sheria zinazo wahusu watoto ,Wazazi,Mirathi,Migogoro ya Aridhi pamoja na Kufahamu namna watakavyo weza kusimamia rasilimali za familia na Taifa kwaujumla.
Kwaupande wake mkurugenzi wa shirika hilo PR. Denis Sinene amesema jukumu kubwa walilo nalo nikuhakikisha watanzania wanapata haki zao Watoto na jamii kwaujumla shabaha kubwa ikiwa kwa Watoto na Mama
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi KISINGA Tulumbe Kyando ametoa Rai kwa wanafunzi ,Walezi na Walezi kutoa ushirikiano kwa taasisi zinazo toa misaada ya kisheria ilikufanikisha Malengo Endelevu ya Kudumu ya Umoja wa Mataifa.
Shirika la mapao wilayani Makete limeendelaea kutoa elimu kwa wanafunzi dhidi ya haki zinazo wahusu pamoja na jamii nzima.
Leave a comment