Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 Sura ya 3
kifungu cha kwanza inasema Kumtunza na Kumlinda Mtoto, Sheria hii inasema
kwamba Mtoto anahitaji huduma na Ulinzi, Iwapo Mtoto huyu.(a) Niyatima au Ametelekezwa na ndugu zake(b) Ameachwa au
anatendwa vibaya na mtu ambae anamtunza na kumlea mtoto au na mlezi au wazazi.
Navifungu vingine vinavyoendelea kwenye sheria hii , Jeshi la Polisi Sudani kusini limeamua kuanzisha mafunzo
maalumu kwa maafisa wa jeshi hilo jisigani watamlinda Mtoto kwenye maeneo yote
yanayo kabiliwa na migogoro.
Maafisa 23 wa jeshi la polisi la Sudan Kusini wanaohudumu
kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo cha
UNMISS wamekutana kwa ajili ya mafunzo maalumu ya kuwalinda
watoto katika sehemu za migogoro.Ni wakati wa kujitambulisha mjini
Juba kwa maafisa hao walio na jukumu la kuwalinda watoto. Wametoka
sehemu tofauti za Sudan Kusini kwalengo la kujifunza mbinu bora
za kuwalinda watoto, kama anavyosisitiza kamishna wa polisi wa
UNMISS, Bi. Unaisi Lutu Vuniwaqa.
“ Tunaona
umuhimu wa kuwamulika watoto, hususan waathirika wa makosa ya
jinai, watoto kama mashahidi, na watoto kama washukiwa pia. Kuna haja
kwetu kupigia debe uimarishaji wa mifumo ya sheria , hasa wakati
huu tunaposhirikiana na wenzetu hapa polisi wa taifa la Sudan
Kusini, kwamba tunahitaji kuendeleza haki za
watoto wanapokabiliana na sheria.”
Darasa limeanza, maafisa hao wa polisi wanajifunza kwa makini jinsi
ya kutekeleza kwa vitendo, elimu na
mbinu wanazopata . Aja Ndey Begay Mbye ni mmoja wa maafisa
hao“Najifunza jinsi ya kukabiliana na watoto, jinsi gani ya
kuwahoji, jinsi ya kuwa nao na kuwaonyesha watoto hao mimi ni mama.”
Taarifa hii nikwa mjibu wa Radio washirika ya Umoja wa Mataifa UN RADIO.
UNMISS yawanoa Polisi Sudan Kusini kuhusu ulinzi kwa watoto kwenye maeneo yalio na migogoro.
Leave a comment