Mahema hayo yaliyosimikwa kwenye kambi ya Mabrouka iliyoko katikati
mwa jangwa huko kaskazini-mashariki mwa Syria yanafuatia msaada wa
kibinadamu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,
UNICEF kwa ushirikiano na wadau wake.
Wavuti maalum unaochapisha habari za watoto wa Syria umemnukuu
Joumana ambaye ni mmoja wa watoto walioshindwa kupata elimu ipasavyo
kutokana na hamahama na ukosefu wa maeneo ya kujifunzia tangu mwaka
2012 walipokimbia kijiji chao.
“Kwa miaka kadhaa kipaumbele chetu kimekuwa ni kuishi,” amesema
Joumana ambaye kabla ya kujengewa mahema matano ya shule walilazimika
kutumia hema moja tu ambalo halikuwa rafiki kwa kujifunzia.
Elimu inayotolewa kupitia mahema haya matano, ni ya kumwezesha mtoto
kujifunza mwenyewe ikilenga zaidi watoto waliokosa masomo kwa muda mrefu
kama vile Joumana.
UNICEF inasema wafanyakazi wa kujitolea wanashirikiana na watoto hawa
ambapo hadi sasa watoto 3,000 kwenye kambi ya Mabrouka wamenufaika.
Joumana anasema, “sikuamini kabisa mwanzoni, wala sikuweza kupata picha mimi niko darasani.”
Tayari Joumana alifanya mtihani wa awali na kupangiwa kujiungana
darasa la 6 akisema kuwa “shule haitufundishi tu masomo bali pia tabia
na mbinu za mawasiliano na kujenga upya jamii zetu.”
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Syria mwezi Machi mwaka
2011 na hadi sasa hakuna mwelekeo wowote wa kumalizika huku watoto
wakisalia kuwa wakimbizi wa ndani na nje ya nchi yao,Taarifa hii nikwa mjibu radio washirika UN radio kwa maelezo zaidi tembelea https://news.un.org/sw