Zaidi
ya watoto 500 wa mji wa Yambio katika jimbo la Gbudue nchini Sudan
Kusini ambao awali walikuwa wanasomea chini ya miti sasa mwelekeo wao wa
elimu umenyooka baada kufunguliwa kwa jengo jipya lenye vyumba vinne
vya madarasa.

Jengo
hilo la shule ya chekechea na ya msingi ya United, kwa kiingereza
United Nursery and Primary Schoo, limejengwa na ujumbe wa Umoja wa
Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS kupitia mradi wa
kuleta matokeo ya haraka, au Quick Impact.
Lucy Samuel ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa darasa la nne katika
shule hiyo amesema amejawa na furaha kwa sababu wamejengewa shule nzuri
ya wao kujifunzia.
Taarifa ya UNMISS imesema shule hii ilianza mwaka jana ikiwa na
wanafunzi 180 wakisomea chini ya miti ambapo hivi sasa imepiga hatua na
idadi ya watoto wanaojiunga kutaka kusoma ikiongezeka hadi kufikia zaidi
ya watoto 500 Taarifa hii ni kwamjibu wa radio washirika UN radio.