Ukatili
dhidi ya watoto ni lazima ukomeshwe mara moja, hakuna visingizio tena.
Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na
Afrika Kaskazini wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
UNICEF.

Geert
Cappelaere ametoa wito huo kufuatia shambulizi la anga lililotokea leo
nchini Yemen na kukatili maisha ya watoto wengi na wengine kujeruhiwa
katika mjini wa Sa’ada Kaskazini mwa Yemen.
Cappelaere ametoa wito huo kufuatia shambulizi la anga lililotokea leo
nchini Yemen na kukatili maisha ya watoto wengi na wengine kujeruhiwa
katika mjini wa Sa’ada Kaskazini mwa Yemen.
Cappelaerre amesema shambulio hilo dhidi ya basi lililokuwa na
wanafunzi ni la kusikitisha na kuhuzunisha , na watoto wote hao
wamearifiwa kuwa na umri wa chini ya miaka 15 huku duru zikisema makumi
ya watoto wameuawa katika shambulio hizo.
Akisistiza umuhimu wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto amehoji “kweli
dunia inataka kupotea zaidi kwa maisha ya watoto wasio na hatia ndio
wakomeshe vita hivi vya kikatili dhidi ya watoto Yemen”?
Amezitaka pande zote kinzani katika mzozo wa Yemen kuheshimu haki za kimataifa za binadamu zikiwemo za watoto. hii nikwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa.