Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka walimu walioshiriki mafunzo ya kujengewa
uwezo wa kumudu Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK) kuonesha umahiri
unaotakiwa katika kufundisha Stadi hizo ili kuleta mabadiliko chanya miongoni
mwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili pindi watakaporejea katika vituo vyao vya kazi.

Waziri Ndalichako ameyasema
hayo mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo hayo ambapo amesema pamoja na
mambo mengine ana imani kuwa kupitia mafunzo hayo walimu wa darasa la kwanza na
la pili wameongeza mbinu ambazo watazitumia kuwafundishia wanafunzi waweze
kumudu stadi hizo kwani ndio msingi bora wa kumudu masomo yanayofundishwa
kwenye darasa la tatu hadi darasa la saba.

“Nyumba
imara hujengwa na msingi
imara hivyo mafunzo haya ni muhimu sana kwenu walimu mnaofundisha Darasa
la kwanza na la pili ili muweze kuwaandaa wanafunzi kumudu vyema masomo
katika ngazi za Elimu
zinazofuata” Alisisitiza Ndalichako