Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, inasema nusu ya wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 15 duniani kote -sawa na watoto milioni 150 – wanaripoti kuwahi kunyanyaswa na wenzao shuleni.
Ripoti hiyo iliyopewa jina, Somo la Kila siku: #KomeshaUkatili katika Shule inasema kuwa unyanyasaji wa rika unaopimwa kwa idadi ya watoto wanaoripoti kunyanyaswa mwezi uliopita au wamehusika katika ugomvi mwaka jana ni sehemu ya matukio katika maeneo ya masomo duniani kote na inaathiri elimu na maisha katika nchi tajiri na hata zile maskini.
“Elimu ni ufunguo wa kujenga jamii za amani, na bado, kwa mamilioni ya watoto duniani kote, shule si salama,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Henrietta Fore. Akiongeza kuwa “Kila siku, wanafunzi wanakabiliwa na hatari nyingi, ikiwa ni pamoja na mapigano, shinikizo la kujiunga na makundi, unyanyasaji wa ana kwa ana na pia mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia na vurugu za kutumia silaha.”
Kwa muda mfupi hii inaathiri mafunzo yao, na kwa muda mrefu hii inaweza kusababisha msongo wa mawazo, wasiwasi na hata kujiua. Vurugu ni somo la kukumbukwa ambalo hakuna mtoto anayestahili kujifunza.”
Ripoti hiyo inaelezea njia mbalimbali ambazo wanafunzi za kuwanyanyasa wanafunzi hao ikiwemo darasani:
Kote duniani, zaidi ya mwanafunzi mmoja kati ya watatu wenye umri wa miaka 13 hadi 15 wamewahi kunyanyaswa , na kiasi kama hicho pia kuumizwa kimwili. Taarifa hii nikwamjibu wa radio washirika UN radio.