wa siku tatu unaonagazia hatima ya watoto walio maskini zaidi barani
Afrika umeng’oa nanga hii leo katika mji mkuu wa Uganda Kampala.
huo umewaleta pamoja watalamu 50 kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa
ajili ya kudurusu hatua na mikakati ambayo imekuwa na manufaa makubwa
kusaidia watoto walio maskini zaidi barani Africa.
Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Dr. Doreen Mulenga, Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia watoto, UNICEF, Uganda
alionyesha matumaini kuwa mkutano huo utaweka bayana hatua muhimu ambazo
zitaleta nuru katika maisha ya watoto waliomaskini Zaidi barani Africa.
Akiongeza kwamba watahakikisha mifano ya mikakati muhimu
itakayobainishwa inatekelezwa nchini Uganda ambako asilimia 55 ya watoto
walio chini ya umri wa miaka 5 wanaishi katika umaskini wa aina tofauti
huku wakinyimwa huduma na haki za msingi mathalani afya, elimu maji,
usafi na malazi.
Dr. Mulenga alibainisha kwamba ukosefu huo huwatia hatarini kunyanyaswa, na kuathiri vibaya mustakbali wao.
UNICEF imeandaa mkutano huo katika ushirikiano na Kituo cha Utafiti
wa Sera ya Kiuchumi (EPRC). Mkurugenzi Mtendaji wa, EPRC, Dr. Sarah
Ssewanyana anatumai kuwa mkutano huu utasaidia watunga sera kuhakikisha
kwamba watoto waliomaskini zadi wameondolewa kutoka umaskini huo na
athari zake.
Taarifa hii nikwa mjibu wa radio ya umoja wa mataifa.
I think this is an informative post and it is very useful and knowledgeable. therefore, I would like to thank you for the efforts you have made in writing this article. KIU