la unyanyasaji au uonevu dhidi ya watoto ni changamoto kubwa ya
kimataifa. Na hii leo changamoto hio imepewa uzito mkubwa katika mjadala
uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York
Marekani.
Mjadala
huo unaofuatia ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uonevu
dhidi ya watoto umejikita katika kutafuta mbinu za kuwalinda watoto
dhidi ya uonevu huo hususan mashuleni.
Ukiwa umeandaliwa kwa pamoja na ofisi ya mwakilishi maalum wa Katibu
Mkuu kuhusiana na kuwalinda watoto dhidi ya uonevu, uwakilishi wa kudumu
wa Mexico na Lithuania kwenye Umoja wa Mataifa , shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na shirika la Umoja wa Mastaifa la
elimu , sayansi na utamaduni, UNESCO umetathimini hatua ambazo
zimeshapigwa katika kulinda haki za watoto na vilevile kuangalia maeneo
ambayo bado yanahitaji jitihada zaidi ili kuhakikisha watoto wanalindwa
dhidi ya uonevu.
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu Bi. Marta Santos Pais amesema tatizo
hilo la unyanyasaji kwa watoto ni baya sana na akatoa mfano wa
kuonyesha uzito wa tatizo hilo katika jamii,
“Miaka kadhaa iliyopita kimsingi tulifanya utafiti na
UNICEF, kupitia mtandao ili kuelewa jinsi watoto wanavyoitizama hatari
hii, tisa kati ya kumi wanaonyesha kuwa hili ni suala nyeti katika
maisha yao na theluthi mbili wamewahi kukutana na manyanyaso ya namna
fulani, na wengine hawakuwahi kumwambia yeyote Kwa kuwa inachukuliwa
manyanyaso hayaepukiki na ni sehemu ya makuzi”
Aidha amesema kitu muhimu kabisa ambacho watoto zaidi ya asilimia 90
wamesema katika utafiti huo ni kuwa, kulindwa kwa watoto dhidi ya
unyanyasaji ni haki muhimu ya binadamu.
Taarifa hii nikwa mjibu wa radio ya umoja wa mataifa, news.un.org/sw.