Usemi unao semwa kwamba hayawi hayawi sasa yamekuwa, mtoto Rehema Paul ambae awali alikuwa ameajiriwa kazi za nyumbani sasa ameandikishwa katika shule ya msingi Mchikichini iliopo ndani ya manispaa ya Morogoro.
Hii nibaada ya mwajiri wake Herrit Mkaanga ambae alibadili mawazo yake yakuendelea kumfanya binti huyo kuwa mjakazi wake akaamua kumludisha shule kwa gharama zake zote, hata hivyo Bi, Herriet ameamua kuanzisha taasisi yake ya MY HEALTH FOUNDATION mkoani Morogoro inayo saidia kutoa elimu na kuwajengea uwezo mabinti walio pata ujauzito na wakajifungua wakiwa shule na wamekata tamaa kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali wakutengeneza batiki,vikapu,vikoi nk.
SIKUAMINI KAMA LEO NINGEANZA SHULE KWA UMRI HUU.
2 Comments
Ni jambo jema kuelimisha binti umeelimisha jamii lakini ni waajiri wachache wanatambua thamani ya wadada wa kazi za nyumbani.
Asante sana mkuu wangu kwa maoni yako mzuri karibu sana na ninakushuru kuten
mbelea website yetu.