MULEBA KAGERA:
Baadhi ya wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum Wilaya ya Muleba
Mkoani Kagera wameshindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kutokana na
kutokuwa na baiskeli za magurudumu matatu pamoja na gharama za
kuwasafirisha kwenye vyombo vya usafiri kwani shule zilizopo zipo
mbali na makazi yao.
Wakizungumza TKT wakati wakupokea basikeli zenye magurudumu matatu kwa
watu wenye mahitaji maalum mmoja wa wazazi mwenye mtoto Bi. Happnes
Bijanda ambaye anaishi katika kitongoji cha ijabalilo kijiji cha
Karutanga amesema yeye alishindwa kumpeleka mtoto wake shuleni
kutokana na kutokuwa na kipandio yaani baiskeli pamoja na kushindwa
kugaramia gharama za usafiri wa kila siku kwani shule ipo mbali na
makazi yake.
Naye afisa elimu wa elimu maalum Bi. Adelina Tefubilwa anasema katika
Wilaya ya Muleba kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum zaidi ya 460
pamoja na vituo vitano vya kulelea watoto wenye mahitaji maalum na
wamekuwa wakiwatambua watoto hao kupitia viongozi wa vijiji na kata
hivyo amewashauri wazazi na walezi kuachana na mawazo duni ya
kuwaficha watoto wenye mahitaji maalum majumbani.
Akitoa baiskeli hizo Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya Wilaya ya
Muleba Bw. Emmanuel Sherembi amesema wamegawa jumla ya baiskeli 11 kwa
watoto wenye mahitaji maalum zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni tano na
laki tisa kwani halimashauri hiyo itakuwa inagawa baiskeli kwa
kusaidiana na wahisani mbalimbali kuhakikisha watoto hao wanatimiza
ndoto zao, Jambo hili linaunga mkono kwenye malengo ya kudumu ya umoja wa Mataifa hususani lengo namba nne (4) linalosema Elimu bora kwa kilamtu SDGs. Na Shafiru Yusuph.