Jamii
wilayani Karagwe mkoani Kagera imesikitishwa na kitendo cha watoto wawili
mapacha wanaokadiliwa kuwa na umri miaka miwili jinsia ya kike
kutelekezwa na mama yao katika stendi ya mji mdogo wa Omurushaka kata ya
Bugene wilayani karagwe.

Akizungumuza
na TKT radio katika eneo la tukio lililotokea
mapema mwezi huu afisa usitawi wa jamii wilayani Karagwe Owokusima Kahiyura
amesema kuwa watoto hao wawili ambao ni mapacha jinsia ya kike wanasadikika
kuwa na umri wa miaka miwili na walitelekezwa na mama yao mzazi katika stendi
ya magari mji mdogo wa Omurushaka
kata ya Bugene wilayani Karagwe kisha mama huyo kutokomea kusikojulikana.

Aidha baada
ya wananchi kubaini kuwa mama huyo ametelekeza watoto hao walitoa taarifa kwa
mwenyekiti wa kitongoji cha Omurushaka C
kisha naye kutoa taarifa kituo cha polisi Nyakahanga na kubainisha kuwa wao
kama ofisi ya usitawi wa jamii watoto hao watawapeleka kituo cha kulelea watoto
yatima Ntoma halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera huku jitihada za
mama aliyefanya tukio hilo zikiwa zinaendelea kufanywa ja na jeshi la polisi.

Hata hivyo tukio hilo ni la pili kuripotiwa
kwa kipindi cha mwaka huu wilayani humo kwani katika kipindi cha mwezi
juni mwaka huu mtoto mmoja alikutwa ametelekezwa katika shimo la
choo mjini Kayanga.

Hata hivyo
nao baadhi ya wananchi akiwemo Linus Kishenyi na Ashura Ghaibu wamesema
kuwa tukio hilo ni la kikatili na kusema kuwa kinachosababisha matukio ya
kutelekezwa kwa watoto wilayani Karagwe ni kutokana na baadhi ya wazazi
kuzaa watoto na kuwatupia mzigo wanawake kwa kukwepa majukumu ya kutoa mahitaji
ya kulea watoto ni pamoja na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi kwani baadhi yao hutokea
katika nchi hizo kama wakimbizi ili kutafuta vibarua kutokana na ugumu wa
maisha.Na Jovinus Ezekiel.

Kinamama wenzangu tujitahidi kuwahurumia watoto tuliowazaa maana sisi ndo wenye uchungu zaidi ya baba zao! Kuna madhara makubwa sana kijamii, kimwili, kisaikolojia na kiroho yanayotokana na kukataliwa kama ambavyo tunawakataa kwa kisingizio cha ugumu wa maisha!?!! …TUFE NAO!!!
Hongera sana dada kwa maoni yako mazuri.