Wanafunzi
wa kike katika shule za msingi na sekondari katika kata ya UFUKUTWA wilaya ya KALIUA mkoani
TABORA wameiomba serikali kupitia
wizara ya elimu kutenga bajeti ya kununua na kuzigawa mashuleni taulo za
kujisitili wakati wa hedhi ili kuinua taaluma kwa mtoto wa kike, Wakizungumza
kwenye kikao kilichowakutanisha wazazi wa kike pamoja na wanafunzi wa kike wa
shule ya sekondari UFUKUTWA na shule
zote za msingi katika kata ya UFUKUTWA
baadhi ya wanafunzi wameeleza adha wanazozipata wakati wa hedhi ikiwa pamoja na
kukosa baadhi ya vipindi darasani hali inayopelekea kushuka kitaaluma.

Kutokana na changamoto hizo wameiomba
serikali kuweka mkakati wa kusambaza taulo hizo katika shule za msingi na
sekondari, ilikuendelea kuwasaidia mabinti hao, Madamu SANGA ni mwalimu
wa malezi shule ya sekondari KAPUYA amewataka wazazi wa kike kuwa karibu na
watoto wao hasa wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi waweze kuwasaidia mengi
yanayo wasibu, Hatahivyo afisa mtendaji
wa kata ya UFUKUTWA, HAPPINESS MASENGWA
amesema kwa kushirikiana na wazazi wamekubaliana kutoa shilingi elfu moja kwa
kila mzazi mwenye mtoto kwa ajili ya kununua taulo za kike.

Nao baadhi ya wazazi wamesema wataweka hamasa
ili kufanikisha makubaliano ya mchango huo,Katika kikao hicho wanafunzi
wamepata elimu ya athari za mimba za utotoni na namna ya kuboresha elimu kwa
mtoto wa kike ambapo waelimishaji mbali mbali wakiwemo dawati la jinsia wilaya
ya KALIUA, Afis a usitawi wa jamii na viongozi wengine wa serikali wamepata
wasaa wa kutoa maada zao. Na Simon Jumanne kutoka KALIUA mkoani TABORA.