Wanafunzi katika shule ya msingi USHOKOLA
wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wamewaomba wazazi kuchangia
chakula kwa ajili ya wanafunzi. Wakizungumza na TKT RADIO Wanafunzi wamesema kutokana na kukosekana kwa chakula shuleni
hapo wamekuwa wakipata changamoto wakati wa vipindi ikiwa pamoja na kutokuelewa
vizuri waalimu wanapofundisha.
Mwalimu AMINA MKUMBO ni mhasibu katika shule ya msingi USHOKOLA
amesema mpango wa chakula haupo kwa sababu ya shule hiyo kukabiliwa na
changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa jambo linalosababisha wanafunzi
kuingia kwa shifiti.

MKUMBO amewataka wazazi kujitokeza na kushiriki ujenzi
wa miundombinu ya shule ambapo kwa sasa shule ina jumla ya vyumba kumi na mbili
vya madarasa, Katika kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni
hapo afisa mtendaji wa kata ya USHOKOLA, MOHAMEDI MUSHI amesema wamekubaliana
na wazazi kuanza mchango kwa ajili ya ujenzi.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema watashiriki
kikamilifu kutoa mchango ili kuongeza vyumba vya madarasa shuleni hapo na
kuanza kutoa chakula kwa wanafunzi. Na Simon Jumanne.

Wazazi na walezi bado tuna wajibu mkubwa wa kufanya hakika