Akizungumza baada ya semina ya kutetea na kupinga ukatiri wa
kijinsia kwa makundi yasiyojiweza iliyofanyika katika halimashauri ya
Wilaya ya Muleba Mkoani kagera Mkurugenzi msaidizi kutoka Wizara ya Katiba na
Sheria hapa nchini Bi. Felicia Joseph amesema kuwa hadi sasa Wizara hiyo
imeishasajiri mashirika yanayotoa msaada wa kisheria zaidi ya 90 pamoja na
wasaidizi wa kisheria zaidi ya 400 hivyo inatakiwa kutoa haki na kujiepusha
vitendo vya Rushwa.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa mashirika yanayotoa msaada
wa kisheria hapa nchini Bi.Kristina Ruhinda amesema hadi sasa kwa Mkoa wa
Kagera wameweza kuwafikia wananchi zaidi ya laki moja kwani wamejipanga kulinda
na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia kwa Watoto
hasa Mtoto wa kike ikiwemo kutoa
elimu mashuleni kwa kushirikiana na serikali.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa
wa kagera Brigedia jenerali Marko
Gaguti Mkuu wa wilaya ya Muleba
Mhandisi Richard Ruyango amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo
kuhakikisha wanawachukulia hatua watuhumiwa ambao walitoroka baada ya
kuwafanyia vitendo vya ukatiri wa Watoto
ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Nao baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Kagera
wakiwemo maafisa ustawi wa jamii Bi Rosemary Nicodemas ,Japhert Kanoni na Denis
Daniel wamesema kuwa changamoto kubwa wanazokumbana nazo katika kukomesha
vitendo hivyo katika jamii ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa waanga wa
vitendo hivyo wakiwemo wazazi wa Watoto
wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia Pale kesi inapokuwa
mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua watuhumiwa.