Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii imewezesha uanzishwaji wa vikundi vya malezi katika
Kata mbili za Halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora.
Akizungumza
katika Kata ya Nzega Magharibi Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima
amesema lengo la kuanzishwa kwa vikundi vya malezi katika jamii ni
kuisaidia jamii kupata elimu sahihi ya malezi ili kuondokana na vitendo
vya kikatili.
Hata hivyo Bi. Tausi amesema kuwa jamii inawajibu wa kuhakikisha
kuwa watoto wanapata malezi bora ambayo yatamuweka mbali na vitendo vya
ukatili ambapo kwa sehemu kubwa vimekuwa vikiwaharibu watoto hasa
kisaikolojia.
Ameongeza kuwa Serikali katika kuhakikisha vikundi
hivyo vinapata nguvu ya kutekeleza wajibu wao imekuja na Kitini cha
Malezi ya Familia ambacho kitawasaidia kupata nyenzo muhimu za namna ya
kuwapa malezi bora Watoto katika jamii.
Bi. Tausi amesisitiza kuwa
vikundi vya malezi vitasimama vizuri basi watoto wetu watapata malezi
bora na kuwezesha kuwa na taifa lenye kuwajibika katika kuwajenga watoto
katika malezi.
“Vitendo vingi vya ukatili kwa Wat’s katika
vinafanywa na wazazi/walezi na watu wa karibu hivyo tunahitaji elimu ya
malezi ili kuhakikisha knatokomeza vitendo hivi” alisema Bi. Tausi
Kwa
upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Jinsia na
Watoto Halmshauri ya Mji wa Nzega Bi. Mwajuma Kisoma amesema kuwa
vikundi vya malezi ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha watoto wanapatiwa
malezi bora ambayo yatasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili katika
jamii.
Taarifa hii nikwa mjibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii.