Serikali imeombwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyo
jengwa kupitia nguvu za wananchi,ili kuendelea kuwatia moyo wananchi
wanaojitolea katika ujenzi katika shule za msingi na sekondari.
jengwa kupitia nguvu za wananchi,ili kuendelea kuwatia moyo wananchi
wanaojitolea katika ujenzi katika shule za msingi na sekondari.
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha kagera kata ya
ikunguigazi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Ndg.DAUDI SAMANDITO GOMBO wakati
akizungumza na TKT Radio,Amesema wamejenga vyumba vinne vya madarasa na
serikali ilitakiwa kupaua vyumba hivyo baada ya wananchi kujenga maboma yote.
Aidha
amewaomba wadau wa elimu kujitokeza kutoa misaada ilikuwapunguzia mzigo
wananchi wanaojitoa na akaiomba serikali kutochelewa katika ukamilishaji wa
vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa kupitia nguvu za wananchi.

Hata hivyo mwalimu mkuu wa shulehiyo MAHEBE
CHIGULU,Amesema shule yake ina wanafunzi 1088 idadi ambayo haiendani na idadi
ya vyumba vilivyopo,kwani mahitaji ya vyumba katika shule hiyo ni vyumba 26 na
vilivyokamilika ni vyumba 6 tu.
Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo ndg.PIUS NDULU,Amesema ili
kukamilisha vyumba hivyo wao kama kamati wamejipangia kila mwaka wanajenga
vyumba vinne vya madarasa kwa kupitia michango ya wananchi.
Kwa upande wao wananchi wamesema wao walijitoa vya kutosha katika ujenzi
wa vyumba hivyo,kutokana na umuhimu wa elimu kwa watoto kwa maisha ya badae.
NA NICKIRAUS PAUL LYANKANDO KUTOKA GEITA.