Shirika lisilo la kiserikali la Morogoro Organization for Women,Elders and Chid Support (MOWECS) linalo shughulika na kuhudumia
wanawake,wazee na watoto makao makuu yake yakiwa mkoani Morogoro,limeleta
ahuweni kwa wananchi hususanini maeneo liliko anzisha mradi unao wahusu watoto
unaoitwa Inua Mtoto.
wanawake,wazee na watoto makao makuu yake yakiwa mkoani Morogoro,limeleta
ahuweni kwa wananchi hususanini maeneo liliko anzisha mradi unao wahusu watoto
unaoitwa Inua Mtoto.
Akizungumza
na TKT/UN Radio kandoni mwa hafla ya
kuuzindua mradi huo katika halmashauri ya Morogoro mkurungezi mtendaji Mery
Mafwimbo amesema lengo la kuu la shirika hilo kuwasaidia familia duni,
kwa kuwaundia vikundi kasha kuwaombea mikopo ilikuweza kuendesha shughuli
wanazo weza kuzifanya wao wenyewe kwenye maeneo yao walipo.
Aidha Bi,Mery
amefafanua kuhusu mradi huo, nikunusuru kundi kubwa la watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu,kupitia wazazi na walezi wao wataweza kunusuru hizo kaya
masikini kwa kufanya miradi mdogomidogo ambayo itawasaidia kupata mahitaji
muhimu kwenye familia na kuendelea kuwatunza watoto wao,ambapo shirika hilo
limefanya utafiti wa awali katika kata tano ndani ya halmashauri ya Morogoro
Kihonda,Lukobe,Kichangani,Mkundi na Chamwino wamebaini kuwepo kwa watoto
walemavu kumina nne(14),watoto
yatima (79) na wale wanao ishi na
wazazi wao lakini kwa mazingira magumu familia (150).
Hata hivyo Afsa maendeleo ya jamii kata ya Mkundi Maria
Matandula kwa upande wa serikali amekili kuwepo kwa watoto wengi
wanaoshi kwenye mazingira hatarishi katika kata hiyo, nakuongeza kwamba
wanakutana na kesi nyingi zinazo wahusu watoto wanao randa randa mitaani na
wanapo fuatilia wana gundua wengi kwenye familia zao hakuna malezi shirikishi yanayo
wawezesha watoto kuendelea kubaki nyumbani hata kama familia imeyumba kiuchumi.
Kwabaadhi ya watoto wlionufaika kupewa misaada ya
vifaa vya shuleni Zurfa Kasim na Godfray Gabriel wameshukuru shirika
hilo kwa kuwapatia dafutari,pencel na pen nakuwaomba waendelee kusaidia watoto
wenye mahitaji kamahayo.
Kwaupande wa wazazi waliohudhuria hafla hiyo
wamesema shirika hilo kupitia mradi wake wa Inua Mtoto unaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii hususani kutoa
ushari, kurejesha na kuwaunganisha watoto kwenye familia zao kwa wale ambao
walisha toroka makwao,kwaupande mwingine
Anna Temba amewaomba wazazi na walezi katika familia kuwalea watoto kwa
misingi ya kidini kama maandiko matakatifu yanavyo sema mlee mtoto katika njia
impasayo nae hataiacha hata atakapo kuwa mzee Mithali 22:6.