Wazazi na walezi nchini wamehimizwa kuwaunga mkono watoto wao pindi wanapoonyesha kuwa na vipaji kwa kuviendeleza badala ya kuvipuuza kwa kuwavunja moyo ili waweze kutimiza ndoto zao wakati wote wa masomo ya o na hata baada ya kuhitimu.
Hayo yamesemwa na evelina Mkwangala mkazi wa ipagala jijini Dodoma ambaye ni mama mazazi wa mwanafunzi wa shule ya msingi chadulu baada ya mtoto wake kuibuka kidedea katika kipengele cha nyimbo miongoni mwa vipengele mbalimbali ikiwemo, upigaji kinanda, ngoma, gitaa, mpira wa miguu na nyimbo kwenye mashindano ya kusaka vipaji kwa shule za msingini mkoani humo .
Mashindano hayo ya kusaka vipaji yameandaliwa na mbunge wa Dodoma mjini mh. Anthony Mavunde na kufanyika Desemba 4 mwaka huu katika ukumbi wa Dear Mama yakijulikana kama MAVUNDE TALENT SEARCH 2019 yakiwa na kauli mbiu ya DODOMA YANGU KIPAJI CHANGU yakilenga kuibua vipaji vya watoto na kuvikuza.
Akizungumza na mwandishi wetu Mkwangala alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiwakazania watoto wao katika masomo ya darasani pekee na kusahau uwezo asilia wa watoto wao hali ambayo husababisha kufa kwa vipaji vyao kudidimia ambapo vingeendelezwa wangeweza kupiga hatua kubwa katika maisha yao.
“
Wazazi wanapasawa kuwaruhusu watoto wao wenye vipaji kushiriki mashindano mbalimbali kuonyesha uwezo wao na kutambulika pamoja na kuwatia moyo kuliko kuwakataza kwa kudai kuwa watafeli masomo siyo kweli” alisema Mkwangala.
Kwa upande wake mwanafunzi wa darasa la tano kutoka shule ya msingi chadulu aliyeibuka mshindi Nuru ally alisema amepokea kwa furaha ushindi huo akisema kuwa siri ya mafanikio yake ni uwezo wake wa kuimba , kuzingatia maelekezo aliyokuwa akipewa wakati wote wa mashindano huku akiishukuru familia yake, walimu na wanafunzi wenzake kwa ushirikiano wao hadi kufikia hatua hiyo ya kuibuka mshindi na kuwakilisha shule yao licha ya ushindani mkubwa uliokuwepo.
“
Ningekuwa sijui kuimba ningeshindwa kwa sababu majaji walikuwa wanaangalia sauti siyo nyimbo natamani kuwa muimbaji bora huko baadaye niendelee kuishi kwenye ndoto zangu”. Alisema Nuru.
Naye mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini patrobasi katambi ambapo aliwataka viongozi wengine kuiga mfano huo katika maeneo yao hatua itakayowezesha kuwakuza watoto katika hali ya kujiamini na kusimamia uwezo wao .
Aidha shule zilizoshinda tatu bora kwa kutoa washindi 20 walioshinda katika vipengele hivyo ni shule ya msingi CHADULU iliyoshika nafasi ya kwanza ilizawadiwa shilingi laki tano, nafasi ya pili ilishikwa na shule ya msingi DCT Bishopstar walipatiwa shilingi laki 3 na nafasi ya tatu ilishikwa na shule ya Mlimwa C walipatiwa shilingi laki mbili huku washindi hao wakipewa ufadhili wa masomo katika shule ya ELLEN WHITE INTERNATIONAL SCHOOL iliyopo maeneo ya Nzuguni ambapo mahitaji yao yote yameghramiwa na mbunge huyo wa dodoma mjini Anthony Mavunde.
NA DEVOTHA SONGORWA DODOMA