Kituo cha utayari IBUMBA kilichopo katika kitongoji cha IBUMBA kata ya UFUKUTWA wilaya ya KALIUA mkoani TABORA kinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa huku wananchi wakiombwa kuendelea kutoa michango kukamilisha miundombinu shuleni hapo.
Hata hivyo Afisa mtendaji wa kata ya UFUKUTWA, HAPPNESS MASENGWA amesema serikali inaendelea kushirikiana na wananchi ili kukamilisha vyumba vya madarasa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kutokana na changamoto ambazo watoto wao wamekuwa wakizipata wataendelea kushirikiana na serikali kuboresha miundombinu shule hayo, ilikuboresha sekta ya elimu hapa nchini, maana sio jukumu la serikali pekeyake kuboresha mazingira na miundo mbinu ya shule.
Akizungumza na wananchi wa kitongoji hicho afisa tarafa ya KALIUA, BETHOD MAHENGE amewataka wananchi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ilikuwaingizia kipato cha ziada jambo ambalo litawasaidia kuchangia maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule zinazo wazunguka kwenye maeneo yao.
Na Simon Jumanne Wilaya Ya Kaliua Tabora.