Watoto wengi wenye tatizo la midomo sungura hapa nchini kwa miaka mingi wamekuwa wakikosa fulaha wanapo fikia utu uzima wakiwa na ulemavu huo,maranyingi wamekuwa wanyonge baada ya kuzaliwa tatizo hilo hasa pale wanapo kutana na vijana wenzao au wanapo kuwa kwenye kundi furani la watu ambao hawana ulemavu kamawao nakujiona kana kwamba hawana haki katika jamii lakini kumbe sio hivyo nisawa na jamii yawatu wengine.
Aidha jopo la madaktari bingwa kutoka shirika lisilo la kiserikali la the Same Qualities Foundation (SQF) Wakishirikiana na uongozi wa hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameanza kambi ya upasuaji bure kwa watoto wenye ulemavu wa midomo sungura katika mkoa huo.
Akizungumza na Tanzania Kids Time (TKT) Mkurugenzi wa shirika hilo Dr.Peter Mabula amesema kwa mara ya kwanza SQF imefanya kambi kanda ya ziwa huku ikikusudia kuendelea kusambaza huduma kama hiyo kwa Tanzania nzima ilikuwaongezea fulaha watoto wenye ulemavu kama huo.
Awali SQF imekuwa ikitoa huduma hizo katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida , ambapo mpaka sasa imekwisha hudumia watoto wapatao 500 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Hata hivyo popote taasisi hii inapotoa huduma zake kamahizi , mgonjwa au mzazi hapaswi kulipa chochote kwani ni bure kabisa, hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Dr.Peter Mabula.