Licha ya Shule ya Sengerema Seminary iliyopo Wilayani Sengerema mkoani Mwanza kushika nafasi ya tano kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 imejipanga kuhakikisha inashika nafasi ya kwanza kwa mwaka 2020.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule hiyo Padree Frances Bonamax Mganyizi wakati akizungumza na TKT/UN RADIO ofini kwake Mjini Sengerema amesema matokeo wameyapokea kwa furaha kwani kwa mwaka imefanikiwa kutoa mwanafunzi bora kitaifa ambapo amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Erick Mtasingwa ambaye amekuwa nafasi ya tatu kitaifa.
Aidha mkuu washule hiyo ametaja malengo walio nayo kuhusu kuendelea kuweka mikakati ilikuhakikisha shule hiyo inashika nafasi ya kwanza kitaifa kwani jambo hilo linawezekana kwa juhudi za kusimamia nidhamu na kuwahimiza watoto kujisomea.
Katika hatua nyingine Padree Mganyizi ameshauli wazazi na walezi kuhakikisha wanawalea watoto kwa kuzingatia maadili huku akiwataka walimu kuendelea kusimamia nidhamu kwa wanafunzi ili waweza kufanya vizuri kweny mitihani yao.
Hata hivyo shule ya Sengerema Seminary imewahi kushika nafasi ya kwanza kitaifa mwaka 2000 na imeendelea kuilinda heshima hiyo kwa kusalia kwenye kumi bora kwa miaka kadhaa.
Na;Deborah Maisa/