Mbunge
wa Jimbo la Morogoro mjini Abdulazizi Abood, amewatembelea watoto
waliolazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, baada ya kufika
ili kuona mashine ya kisasa ya kutoa huduma ya X- Ray iliyoletwa na
serikali ili kuwasaidia wananchi wakiwepo watoto mkoani humo.

Ziara
hiyo ya kutembelea hospitali hiyo imefanyika hivi karibuni na baada ya hapo
amevitembelea vituo vya Afya katika Manispaa ya Morogoro huku ameishukuru Serikali, kwa
kutekeleza ahadi yake hiyo na kuwajali wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa
kuleta mashine ya kisasa kwa ajili ya huduma za X-ray kwani kilikuwa ni
kilio Cha muda mrefu ambacho amekuwa akiiomba Serikali kuwasaidia kifaa
hicho. .

Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Dkt. Ritha Lyamuya alisema kuwa, mashine hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kazi hali ambayo imesaidia,kupunguza malalamiko ya wagonjwa ambao walikuwa wakikosa huduma ya X-ray kutokana na mashine iliypokuwepo awali kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi.
Alisema
mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi na hivyo kusaidia,
kupunguza idadi ya wagonjwa ambao, walikuwa wakipewa rufaa kwenda
hospitali ya Taifa Muhimbili, kwani mashine hiyo ina uwezo wa kutuma
taarifa za mgonjwa kwa njia ya mtandao na kurejesha majibu ndani ya muda
mfupi.

Na Shua Ndereka, Morogoro.