Baadhi ya shule katika halmashauri ya wilaya
ya bukoba vijijini mkoani kagera bado ni changamoto kubwa hayo yamebainishwa
katika baraza la madiwani wa halmashauri hiyo .
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwa
afisa mipango wa halmashauli hiyo Bwana JULIAN TALIMO wakati akiwasilisha
rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 20202021 ambapo amesema katika mwaka huu wa
fedha changamoto hii ya uhaba wa vyoo itatatuliwa kulingana na fedha inayotarajiwa
kurasimishwa katika halmashauri.
TALIMO ameeleza zaidi ya bilioni 56 na zaidi
inategemewa kurasimishwa huku bilioni 5.8 inatarajiwa kuelekezwa katika miradi
vipolo na ujenzi ikiwemo ujenzi wa matundu ya choo katika shule ili kuwanusuru
watoto katika changamoto hiyo.
Hata hivyo amesema halmashauri BUKOBA
vijijini ilitegemea kuandikisha watoto wa elimu ya awali jumla ya wanafunzi 11,933
huku asilimia 79% ya watoto walioandikishwa wamekumbwa na uhaba wa vyoo
mashuleni.
Nae afisa elimu sekondai Halimashauri
hiyo Bwana, CHACHA MEGEWA ameongeza kua licha ya kuwepo kwa changamoto ya vyoo
mashuleni lakini pia kuna changamoto ya wanafunzi kupata mimba kabla ya
kumaliza elimu yao.
CHACHA
amesema wanafunzi waliotambuliwa kupata mimba kwa upande wa sekondali wapo 18
kwa mwaka uliopita huku kwa mwaka huu sasa inakadiliwa zaidi ya wanafunzi
10 tayali wamebeba mimba katika shule mbalimbalindani ya halmashauri
hiyo.
Na Silvia Amandius.