Utekelezaji
wa Elimu Jumushi katika kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera
bado ina changamoto hasa Shule ya msingi Nyabushozi ambayo mazingira yake si rafiki
kwa watoto wenye ulemavu wa viungo.

SILIVIA
AMANDIUS ni mwandishi wa habari za watoto kutoka TKT/UN RADIO ametembelea
nyumbani kwa ASHRAFU YASINI ambaye ni
mlemavu wa miguu, pia ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Nyabushozi,
iliyopo kata ya Butelankuzi mkoani
KAGERA.

Licha
ya ulemavu huo ASHRAFU anatembea umbali mrefu kwa takribani kilometa tano,
kufuata masomo shuleni, akitumia magongo (fimbo) ili kumsaidia kutembea vizuri,
ameiomba serikali kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi.
“Naomba
msaada wa baiskeli, natoka nyumbani naanguka pia nachelewa shuleni..” Alisema
Ashirafu.

ya changamoto hiyo ASHRAFU anasoma kupitia mpango wa serikali wa elimu jumuishi
ambao huwawezesha watoto wote kusoma katika shule moja na katika mazingira ya
aina moja bila ya kuwabagua watoto wenye
mahitaji maalumu, pamoja na wenye ulemavu ambapo Mkuu wa shule ya msingi Nyabushozi ALFRED
JONATHAN amesema mazingira ya shule hiyo siyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu
wa viungo.
Pia
ameeleza kuwepo kwa changamoto shuleni hapo kuwa wanafunzi wengi wenye ulemavu,
hukabiriwa na masuala ya utoro kutokana na miundombinu shuleni siyo rafiki.
“miundombinu
ya shule siyo rafiki kwake Ashirafu, kwani madarasa yana ngazi ndefu hawezi
kupanda kwa haraka pamoja na miundombinu
ya vyoo si rafiki”. Alisema Alfred Jonathan.

TKT/UN
RADIO imezungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Nyanushozi, DAUDA KATUNZI ambaye
ameelezakuwa, bodi yake ndiyo inayohusika na michakato ya maboresho ya shule,
ikiwemo ujenzi wa miundombinu pamoja na kuletewa ramani kutoka halmashauri, hivyo wao wanakuwa
hawajui wala kubadilisha chochote.
Kulingana
na changamoto anazopitia ASHRAFU shuleni na nyumbani, mamayake NADHIFA YASIN
amesema katika kijiji chao, dhana ya ulemavu bado inatazamwa kama mkosi na licha
ya hali duni ya maisha aliyonayo lakini anaamini kupitia mpango wa Elimu
jumuishi mtoto wake atafika mbali.
“kuanzia
darasa la kwanza nilikuwa nampeleka kwa baiskeli shuleni lakini niliugua……mtoto
wangu anateseka sana katika kuitafuta elimu, na anania ya kusoma….” Alisema
Mama Ashirafu.

Kwa
mujibu wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Tanzania imeridhia
matamko mbalimbali ya kimataifa ambayo yamelenga kuinua elimu jumuishi shuleni,
miongoni mwa matamko hayo ni tamko la Haki za Watoto, tamko la Haki za Watu
wenye Ulemavu lililotolewa tangu
mwaka wa 1974.
Katika
mahojiano ya TKT/UN RADIO, Watunga sera na Wasiamizi wa elimu katika kata ya
Butelankuzi na Halamshauri ya Bukoba wamekiri kuwepo kwa changamoto na kubainisha
kuwepo kwa baadhi ya viongozi wasiotekeleza maelekezo ya serikali katika uboreshaji
wa sera husika.

Diwani
wa kata ya Butelankuzi, GASPAL MASHONGOLE amesema wanafunzi wanapaswa kupewa fursa
sawa ya elimu na kutengenezewa miundombinu bora kwa ajili ya mahitaji maalumu
hasa watoto wenye ulemavu.

Hata
hivyo Mwanasheria wa kujitegemea JOVIN RUTAINULWA amesema kwamba, kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezungumzia haki za binadamu
ikieleza haki ya mtu kutobaguliwa kwa hali yake ya kimaumbile, rangi au kabila
lake.

“Serikali
inapaswa kujenga mazingira mazuri ambayo yatawasaidia watoto kupata huduma
kulinga na hali yao kwa watu wenye ulemavu na wasiona ulemavu” alisema Jovin

hivyo Elimu Jumuishi kwa Maendeleo ya Elimu kwa Wote Tanzania, imejengwa katika
msingi wa haki za binadamu, yaani kila binadamu ana haki ya kujumuika na kupata
mahitaji yake kamilifu akiwa ndani ya jamii bila kutengwa wala kubaguliwa.

Na; Silivia Amandius, Kagera.
Kwa kweli selikari inahitajika kuliona Jambo Hilo na kulitilia mahanani.
Bilashaka.