Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Njombe imeweka
mikakati ya kupunguza kesi za ubakaji, ulawiti na ukatili kwa kusikiliza
mashauri ya watoto ili kudhibiti njia za rushwa miongoni mwa wazazi na
watuhumiwa.

Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa
Njombe HASSAN MAKUBE amesema tabia ya
baadhi ya wazazi kuweka vikao vya kumaliza kesi za ubakaji nyumbani
imesababisha mahakama kushindwa kuwatia hatiani watuhumiwa.

Amesema hali
hiyo inasababisha mashahidi wa kesi za
ubakaji na ulawiti Kushindwa kuhudhulia mahakamani kutoa ushahidi na kuchangia
watuhumiwa kuachiwa huru pasipo haki ya
mtoto kupatikana.

MAKUBE
amesema Matukio ya ubakaji na
ulawiti asilimia kubwa yanafanywa na
wanandugu ambao wamekuwa na vikao
vya kumaliza kesi hizo nyumbani na watuhumiwa kutoa fedha kinyume na sheria ili
mashahidi wasifike mahakamani.

Kaimu mkuu wa Takukuru Mkoa wa Njombe ALFEO LUNGWE amekili kuwepo
changamoto ya wazazi kushiriki vikao vya kumaliza kesi za ukatili kwa watoto
nyumbani na kupokea fedha kwa watuhumiwa huku akikemea vikali tabia hiyo ambayo
inakwamisha maendeleo ya utoaji hukumu za kesi mahakamani.

Nae Mtendaji Wa Mahakama Mkoa Wa Njombe YUSUPH
MSAWANGA akizungumza na kituo hiki, amesema ili kudhibiti na kutoa haki za
watoto mahakamani, jamii inapaswa kukemea tabia za wanandugu kuendekeza vikao
vya kumalizia nyumbani kesi za ubakaji wa watoto badala yake waiachie mahakama
itende haki huku akiomba kuongezwa mahakama vijijini.

Kwa upande wa wananchi mkoani Njombe wamesema vitendo vya ubakaji kwa watoto
vinafanywa na wanandugu pamoja na baadhi ya akina baba wenye imani potofu za kishirikina
zinazowataka kubaka watoto ili kupata utajiri
huku wakitaka vyombo vya sheria kutunza siri za watoa taarifa za
ukatili.

Na Michael
Ngilangwa-Njombe.
Ngilangwa-Njombe.