Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare, amewapongeza wadau kwa kufanikisha
ukarabati wa madarasa chakavu katika shule ya Msingi Mji Mkuu iliyopo katika
Halmashauri ya Manispaa ya ,Morogoro.
Pongezi
hizo amezitoa wakati wa ukaguzi wa madarasa Manne chakavu yaliyokarabatiwa
chini ya ufadhili ambapo madarasa mawili yametokana na ufadhili wa Mhe.
Abdulaziz Abood Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kupitia mfuko wa jimbo na
mengine mawili chini ya ufadhili wa Nashela Hotel.

Katika
ukarabati wa madarasa hayo ,Mfuko wa Jimbo la Morogoro Mjini uliweza kuchangia
shilingi Milioni 3 na laki 6 na fedha binafsi kutoka kwa Mhe. Abood ni shilingi
Milioni 1 na Laki 4 huku ufadhili wa Nashela Hoteli ukitumia takribani shilingi
Milioni 10.

“Napenda
kutoa pongezi zangu za shukrani kwa wadau wote, haswa Mhe. Abood na Nashela
Hotel, kwakweli shule hii ipo barabarani njiani kabisa nilipiga kelele lakini
leo angalau ilifikia wakati nikamwambia Mkuu wa Wilaya tuifunge shule hii
wanafunzi na walimu tuwahamishe lakini sasa inaonekana kufufuka, niombe
Manispaa iangalieni shule hii kwa jicho la huruma ikiwezekana tafuteni pesa
haraka kukoa jahazi hali sio nzuri viongozi wanapita njia hii ni aibu kubwa
” Amesema Sanare.

Amesema
mikakati yake ni kuhakikisha Watoto wote waliofaulu wanaenda shule na wanakaa
kwenye madawati na atazunguka kila kata kuona hali ilivyo.

Pia
ameendelea kusisitiza kwamba wale walimu Wakuu waliodumu muda mrefu bila ya
matokeo mazuri ya ufaulu watashushwa vyeo na kuwa walimu wa kawaida na Walimu
ambao hawako shuleni bila taarifa za msingi wakatwe mishahara yao pamoja na
kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

amewaagiza Maafisa elimu wasaidiane na Wadhibiti ubora wa elimu ili kuleta
matokeo chanya ya viwango vya ufaulu katika Mkoa wa Morogoro.

“Tunachotaka
ni matokeo, yapo malalamiko mengi shuleni wananchi wanaonewa wakati Serikali
ilishatoa maelekezo lakini hayatekelezwi, hivyo hatutakuwa tayari kuwaadhibu
wadhibiti ubora wakati wapo waratibu wa elimu, niwaombe waratibu wa elimu
wasimamie shule na sitotaka kusikia malalamiko kwani kikwazo cha kwanza katika
kuchangia matokeo mabaya ya elimu ni watendaji “amesema.

Na, Shua Ndereka-Morogoro.