Wazazi wa
watoto wenye ualbino wanaosoma shule ya Msingi Mugeza Mseto iliyopo manispaa ya
Bukoba mkoani Kagera wamelalamikiwa kwa kuwatelekeza watoto wao shuleni.

Mwalimu
mkuu shule ya Msingi Mgeza mseto Bi.Joyce Lobozi amesema hayo wakati
akizungumza na baadhi ya wazazi wanaoishi wilayani Bukoba wakati wa kikao
kilichoandaliwa na chama cha watu wenye ualbino manisaa ya Bukoba kujadili
changamoto wanafunzi wenye ualbino.

Amesema
kuwa wako baadhi ya watoto waliopelekwa shuleni wakiwa na miaka miwili lakini
wamefikia darasa la 5 hadi la 6 bila kutembelewa na wazazi wao na kwamba watoto
hao wanakosa upendo wa dhati kutoka kwa wazazi wao na kujiona watofauti na hata
baada ya wazazi kupigiwa simu wamekua wakidai hawana nauli.

Medianita Mnanuzi
ni mlezi wa wanafunzi shule ya msingi Mugeza mseto amesema kuwa kutokana na kupita
kipindi kirefu bila wanafunzi kuwaona wazazi wao, pindi wanapokutanishwa nao huwakataa
wakiamini walezi ndio wazazi wao.

Baadhi ya
wazazi walioshiriki kikao hicho wameitaka serikali kuwaeliisha wazazi wenye
tabia hiyo ili kuondokana na dhana potofu ya unyanyapaa kwa watoto wao na
kwamba kwa wanaoshindwa kubadilika wachukuliwe hatua kali za kisheria, kwani
hali hiyo humuathiri mototo kisaikolojia.

Katibu wa
chama cha watu wenye ualbino Manisaa ya Bukoba Bwana,Frolence Felician ameeleza
kuwa, kwa kushirikiana na ofisi za serikali waliko wazazi wa watoto hao wamekuwa
wakiwatafuta na kuwapatia Elimu, licha ya kwamba inachukua muda na kwamba
wanalo kusudio la kuendelea kukutana na wazazi kuwapa Elimu mara kwa mara.

Na, Rosemary Eliasi-Kagera.