Vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 15.3
vimetolewa na Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kupitia mapato ya
ndani fedha itakayotumika katika ujenzi na kukamilisha miundombinu kwenye shule
nne za Sekondari.

Akizungumza katika Hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo
iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Afisa Elimu Sekondari
Wilaya Bi,Savelina Misinde amesema kuwa vifaa hivyo ni mabati 490 upande wa
Shule za Msingi wakati mabati 100 kwa shule za sekondari Kagera, ambazo ni Bwanjai,
Bunazi na Bugandika zilizokuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa 6 kwa ajili ya
wanafunzi wa kidato cha kwanza na nyumba ya walimu.

Bi Savelina ameongeza kuwa fedha iliyonunulia vifaa hivyo
imetokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kwamba miundombinu hiyo
ikikamilika itachangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua kiwango cha taaluma

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa Halmashauri
ya Missenyi Bwana, Innocent Mkandara amesema kuwa halmashauri inakusudia
kutatua changamoto ya miundombinu iliyopo kwenye baadhi ya shule za msingi na
sekondari mkoani Kagera na kuitaka jamii kushirikiana na Halmashauri ili
kufanikisha lengo hilo

Baadhi ya wakuu wa shule zilizopatiwa misaada hiyo akiwemo
Donatus Ishengoma mkuu wa shule ya Bwanjai na Steven Kamugisha wa shule ya
Bugandika licha ya kuishukuru Halmashauri kwa msaada huo, wamesema kuwa
miundombinu inayojengwa itasaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani
sambamba na walimu kuishi karibu na maeneo yao ya kazi na kwa pamoja
yatawezesha kukua kwa taaluma.

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo akiwemo Yusuph Amada wa
kata ya Kassambya na Silivia Mwandiki wa kata ya Kyaka wamesema kuwa wananchi
wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kufamikisha shughuli za maendeleo na
kwamba wataendelea kuhamasisha jamii kushirikiana na serikali kutatua
changamoto mbalimbali za kielimu.

Na Rosemary Bundallah-Kagera