KUFUATIA
tukio la kukamatwa kwa Mkazi wa kijiji cha Ngayaki, wilaya ya Gairo
Mkoani Morogoro Bi. Zawadi Kitongo kwa kosa la kukaa kikao cha Mahari ya
binti yake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Mkuu wa Wilaya
hiyo Mheshimiwa Siriel Mchembe amewaonya wazazi wanaoendekeza ndoa za
utotoni.

Mheshimiwa
Siriel ameipongeza kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo, kwa
kufanikisha kuzuia ndoa iliyokuwa inatarajika, kufanyika siku chache
zijazo kati ya Mwanafunzi huyo kutoka shule ya sekondari Madege na Bwana
Julius Mchanya wote kutoka kabila la Wakamba.

Aidha
amesema kwamba, kutokana na uzoefu wa wananchi wanapofanya uhalifu
hujihami hasa wanapoona gari la Polisi ama gari la Serikali ilibidi gari
binafsi litumike, kufanikisha zoezi la kuwakamata wahalifu.

“ilimlazimu
OCD kutumia gari binafsi la askari aliyejitolea ambaye ni CPL Revocutus
Sabwoya, amabaye aliambatana na Askari wa Dawati la Jinsia Hope Tarimo,
askari wengine pamoja na TAKUKURU” amesema.

Kwa
Upande Mwingine Mkuu wa Wilaya Siriel Mchemba amewaagiza wazazi wa
wanafunzi wote ambao hawajaripoti kidato cha kwanza wajisalimishe kwenye
Ofisi za Watendaji kata na vijiji ili kueleza wanafunzi wapo wapi na
baada ya siku saba watakwenda kueleza katika Kituo cha Polisi.

Na SHUA NDEREKA-Morogoro.