TKT/UN RADIO |
Halmashauri ya wilaya ya KALIUA mkoani TABORA imetoa fedha taslimu millioni mia tatu arobaini na tano kwa vikundi 57 vya wanawake, vijana na walemavu huku vikundi vikisisitizwa kurejesha fedha hizo.
Akimkalibisha wakati wa hafla mgeni
rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa TABORA kukabidhi hundi ya fedha hizo mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wilaya ya KALIUA, MWANAHAMISI ALLY ameiomba serikali kuvisisitiza vikundi kurejesha fedha wanazokopeshwa.
TKT/UN RADIO |
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya KALIUA, Daktari JOHN PIMA amesema kuanzia julai 2015 hadi disemba 2019 halmashauri imetoa jumla ya fedha millioni mia nane thelathini na tisa kwa vikundi mia mbili na tisa vya ujasiliamali huku akiongeza kwa kusema fedha hiyo itakayotolewa ni kwa vikundi 57 vya ujasiliamali ikiwa vikundi 28 ni vya wanawake, 19 vijana na vikundi 10 ni watu wenye ulemavu.
Lengo kuu la kukopeshwa fedha hizo nikuongea mitaji kwenye biashara wanazo zifanya ilikuongeza kipato na kukidhi mahitaji ya msingi kwa watoto wao.
Katika hotuba yake mkuu wa mkoa wa TABORA, AGGREY MWANRY amesema licha ya kuipongeza halmashauri ya wilaya kwa kutenga na kutoa fedha kwa ajili ya vikundi amezungumzia pia suala la ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na wakina mama kuwa bado nitatizo katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya KALIUA, ABELI BUSALAMA naye ameipongeza halmashauri ya wilaya kwa kuendelea kutekeleza maagizo ya serikali ya kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya ujasiliamali,nakuwashauri wakina mama waliopo kwenye vikundi pesa walizo zipata sio zakutumia Bali wazifanyie biashara nafaida itakayo patikana iwasaidie watoto kuwatimizia mahitaji ya msingi.
Hata hivyo SOPHIA MBANDILA ni mwenyekiti wa kikundi cha JITEGEMEE amesema fedha wanazokopeshwa na halmashauri zimekuwa zikiwasaidia kuongeza mitaji yao kwa na kuongeza kipato cha families wakiwemo watoto na kujikimu kimaisha kwa Yakima siku.
Na Simon Jumanne, Kaliua Tabora.