Wapo watoto wengi nchini wenye ulemavu wa viungo,wenye ualbino na ulemavu wa akili kwa asilimia kubwa hukosa nafasi ya kupelekwa shuleni kuandikishwa kwa ajili ya kuanza safari ya elimu ambayo itakuwa msaada mkubwa maishani mwao.
Jambo hili huwanyima haki zao za msingi watoto ambao ni wenye ulemavu wanapo shindwa wazazi/walezi wao kuwapeleka kweneye vituo vyakufundisha watoto wenye mahitaji maalum kama Baraka Msungu,ziko sababu kadhaa ambazo ni za kusadikika kuhusu watoto wenye ulemavu,zinazo pelekea kushindwa kuwapeleka shuleni kwa ajili ya kupata elimu, kamavile imani za kishirikina, kudhani kwamba hatakuwa na msaada wowote kwenye familia husika.
Aidha wazazi/walezi wengine hushindwa kuwaamini watoto wao wenye ulemavu kwamba wanaweza kwenda shuleni na wakajifunza kusoma na kuandika,badala yake wanawafungia ndani na kuwazuia kutoka nje ya eneo lao la nyumbani.
Hali hii nitofauti kwa mzazi wa Baraka mkaazi wa kata ya bigwa Manispaa ya Morogoro ambae katika familia yake mke wa Adasi Msungu alijifungua mtoto wakiume awali alikuwa mzima kadri siku zilivyo zidikwenda baraka alibadirika akili yake baada ya kupeleka hospitali wataalamu wa afya wakashauriwa kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afyayake.
Baada ya kumpima akagundurika kuwa anatatizo la utindio wa ubongo, ambapo sasa nimkubwa mwenye umri wa miaka kumi na nne, na wazazi wa baraka wannia ya kumpeleka kumuandikisha shuleni ilikuanza masomo akiwa amechangamana na wenzake kwani hiyo ni haki yake ya kupata elimu na Msungu aliongezea kwa kusema “huu niwajibu wetu wakuhakikisha tunawasomesha watoto wetu wote kila mmoja apate elimu ambayo ndio msaada wao popote waendako tutafanya kwasehemu yetu pale tutakapo weza ilimradi akili yake ichangamke” mwisho wa kumnukuu.
Hata hivyo Nd.Msungu anahitaji kumpela shule ya msingi lakini anakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za matibabu ya mtoto huyo kwani dawa anazo zitumia nigharama kubwa ukilinganisha na kipato alicho nacho yeye mwenyewe, changamoto nyingine niusafiri wa kumbebea wakati wa kwenda shuleni na wakati wa kurudi nyumbani kwani hawezi kumbeba kwenye pikipiki isipokuwa pikipiki ya matairi matatu yaani (bajaji).
Herriet Mkaanga yeye nijirani yake anasema familia hiyo ina hitaji msaada kwa ajili ya mtoto huyo Baraka, kwanza kwaupande wa matibabu yake nilazima kila baada ya miezi mitatu waempeleke kiliniki hospitali ya taifa muhimbili,pili huvalishwa pampasi hadi sasa japokuwa nimkubwa wa umri wa miaka kumi na nne.