Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake
wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Njombe bi. Angela Mwangeni amekemea tabia ya baadhi ya wanaume
kulazimisha kurithi wajane kwani kitendo hicho kinawaathiri watoto kutopatiwa haki zao za msingi.
Bi. Mwangeni ametoa kauli hiyo
wakati wa kukabidhi msaada wa fedha shilingi laki mbili za kununulia baiskeli
ya kutembelea mtoto mwenye ulemavu wa miguu na mtindio wa ubongo Gift Asukulye Kihombo mwenye umri wa
miaka 13 mkazi wa kijiji cha Lole.

Amesema tabia ya kulazimisha
kurithi wajane na kunyang’anya mali za watoto imebainika katika kata ya
Ikuna ambapo imedaiwa kuna mwanaume mmoja ni kiongozi wa chama cha
mapinduzi kata ya Ikuna anajihusisha na tabia hiyo na kuahidi kusimamia ili
mjane huyo asimamie na kuwalea watoto
wake mwenyewe.

Kwa upande wake diwani wa kata ya
Ikuna ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Valentino Hongoli amesema wanawake wajane wanatakiwa kuwa makini na
wanaume wanaotaka kuwarithi kwani wapo wanaowarithi kwa kufuata mali huku
akipongeza wazazi wa Mtoto Gifti Kihombo mwenye ulemavu kwa kushikamana kumlea.

Afisa mtendaji wa kata
ya Ikuna Wilayani Njombe Bi. Alistidia
Nazar amekili kuwepo matukio ya unyanyasaji
na ukatili kwa akina mama wajane na watoto ambapo amesema serikali za vijiji
bado zinaendelea kukemea tabia za kulazimisha kurithi wajene ili kuepukana na
madhara ya watoto kudhurumika mali zao.

Nao wazazi wa mtoto mwenye
ulemavu huyo aliyekabidhiwa msaada wa
fedha hizo kwaajili ya kununulia baiskeli akiwemo mama yake Esteri Sambanaye na
Mme wake bwana Asukulye Kihombo ambao ni wazazi wenye familia ya watoto watano
wameshukuru kusaidiwa msaada huo ambao utawezesha mtoto wao kutembea kwa
kutumia baiskeli.
Akizungumza na kituo hiki afisa
ustawi wa Jamii Wilaya ya Njombe Averino
Chaula amepongeza wananchi kwa kushiriki kukemea tabia za kurithi wajane na
kusaidia watoto wasiyo jiweza ambapo
ametaka moyo huo kuendelea hata kwa kata nyingine wilayani humo.

Jumla ya shilingi laki mbili na tisini zimekabidhiwa
kwa wazazi hao kwaajili ya kumsaidia
kupata baiskeli ya magurudumu matatu mtoto Gifti Asukulye Kihombo mwenye umri wa
miaka 13 ambaye anatatizo la ulemavu wa miguu na mtindio wa ubongo aliozaliwa
nao.