Kufuatia kukithiri kwa
tabia ya baadhi ya wazazi kugoma kabisa kuchangia uji na chakula shuleni kwa
ajili ya watoto wao serikali mkoani Kagera imezitaka serikali za mitaa na
vijiji kuunda sheria za kuwawajibisha wazazi hao ili wanafunzi waweze
kuondokana na changamoto zinazowaata kutokana na kukosa huduma hiyo.

Katibu tawala wa mkoa
huo Prof.Faustine Kamuzola amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kikao
cha ALAT mkoa na kwamba inasikitisha kuona yanakuweo makundi wakati wa
utolewaji wa huduma ya uji shuleni (wanakula na wasiokula) na kwamba kwa
asiyetoa inamuathiri kiasi kikubwa kwani humpunguzia uwezo wa kitaaluma.

Aidha amewaagiza
wanasheria ofisi ya mkuu wa mkoa kuzisaidia serikali za mitaa kuunda hizo
sheria ndogo na kuwasaidia katika michakato yote ya upitishaji ili izingatie
utaratibu kisheria

Awali akiwasilisha
taarifa kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa ALAT mkoa Bw,Kashunju Kanyuguli
ameiomba serikali kuingilia kati utatuzi wa changamoto hiyo kwani wengi wao
bado wanaamini kwamba serikali inatoa kila kitu kupitia elimu bure.

Kwa niaba ya wajumbe
wa kikao hicho William Ruta amesema kuwa kuundwa kwa sheria hizo ndogo na iwapo
zitatekelezwa kwa ufanisi mkubwa zitaleta matokeo chanya kwani wasio toa
watawajibishwa na kama wazazi watatii sheria hizo mafanikio ya kitaaluma kwa
wanafunzi yataongezeka.

Baadhi ya wazazi manispaa
ya Bukoba wameiomba serikali ya mkoa huo kuendelea kuielimisha jamii kuhusu utoafauti wa uchangiaji wa chakula
shuleni na elimu bure badala ya kujikita
kwenye utungaji was Sheria za kuwabana wasio changia.