Madawati miambili (2) yenye thamani ya shilingi milioni 101,000,000 (milioni kumi na laiki moja) yametolewa na chama cha akiba na mikopo cha watumishi wa umma wa halmashauri za Bukoba na Missenyi BHURUTE kunusuru changamoto ya madawati inayozikabiri shule za msingi za halmashauri hizo.
Mwenyekiti wa chama hicho Bw,Gerald Kigundu amesema kuwa moja ya kipengele cha katiba yao ni kutoa misaada kwa jamii na kwamba kila mwaka utenga bajeti kwa ajili ya kuchangia chochote cha maendeleo na wameamua kutoa madawati kwa halmashauri hizo kutokana na changamoto iliyopo.
Akizungumza baada ya halmashauri yake kukabidhiwa madawati hayo kaimu afisa elimu msingi Bw,Mujib Babala amesema kuwa madawati hayo mia 1 yataelekezwa kwenye shule 3 zenye upungufu mkubwa ambazo ni Mwisa, Bugango na Mabale.
Licha ya kukiongeza chama hicho cha BRUTE mkurugenzi wa halmashauri ya Missenyi Bw,Innocent Mkandala amekiri shule za msingi kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawati na kwamba amekuwa akiwasiliana na wadau mbalimbali ili kusaidia katika utatuzi wa changamoto hiyo.
Mgeni rasmi wa afla hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwila akizungumza mara baada ya kukabidhiwa madawati hayo amezitaka asasi nyingine za kiraia kushirikiana na serikali katika utatuzi wa changamoto ya madawati na kwamba chama hicho kikawe mfano kwao.
Na,Rosemary Bundallah-Kagera.