Watanzania watakiwa kufuatilia taarifa mbali mbali zinazo husu homa inayo sababishwa na virusi vya corona kupitia vyombo vya habari kamavile radio,Tv ,magazeti na mitandao ya kijamii ya kuaminika iliopo hapa nchini,ili kuendelea kuchukuwa tahadhari ya maambukizi.
Hayo yamejadiriwa kwenye mkutano ulio andaliwa leo na shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF Tanzania kwa njia ya mtandao,mkutano huo ulikuwa na lengo la viongozi wa dini kuwahimiza waumini wao kufuatilia ibaada wakiwa nyumbani ilikupunguza msongamano na kuendelea kujikinga na kuwa kinga watoto wao.
Aidha Askofu Frederick Shoo wa kanisa la Lutheran Tanzania amesema nilazima kila kanisa nchini liwasaidie waumini wake kuhakikisha yanaweka vitendea kazi vinavyo hitajika kama vile vitakasa mikono na kutoa elimu ya ushauri kuhusu kujikinga, kwani walio wengi wana hofu kubwa kwenye mioyo yao,hivyo viongozi wadini wanawajibu wa kuituliza miyo hiyo wakiwa majumbani mwao.
Hata hivyo kiongozi mkuu wa dini ya Hindu Pujya Swami amewaomba viongozi wadini nchi Tanzania kujifunza mambo mengi kutoka India kwani awali nchiyo ilikuwa na maambukizi ya chini kwa muda walivyo endelea kufanya mikusanyiko mikubwa maambukizi yaliongezeka hadi kufikia idadi kubwa.
Wakati huo Dr.Thabo Makgoba wa kanisa la Anglican Africa ya Kusini amewashauri waumini kutoka maeneo mbalimbali ya nchi waamini kwamba kufanyia ibaada nyumbani siokushuka kiimani kwani nijambo la msingi ili kujikinga na maambukizi, nakuhakikisha kila mmoja anazingatia kanuni za afya zinazo tolewa na wataalamu wa afya.
Kwa upande wake mkuu wa maweasilianao wa shirika la UNICEF kusini mashariki mwa Africa Jemas Eider amesema viongozi wa dini wanategemewa sana ilikuendelea kutoa elimu ya kujikinga na corona pamoja na wazazi wanapaswa kuondoa hofu na kuwasikiliza watoto wao nini wanahitaji kwa wakati huu, nasio kuendelea kuwapa msongo wamawazo kuhusu maambukizi ya corona.