Wakati dunia ikiendelea kuhuzunika na kupambana na maambukizi ya mripuko wa ugonjwa wa corona (Covid-19) mashirika mbalimbali hayakubaki nyuma kwa ajili ya kutoa misaada ya aina mbalimbali ikiwemo ya ulimishaji namna ya kukabiriana na mripuko wa ugonjwa wa corona (Covid-19).
Shirika la Inter-Agency Standing Committee Reference Group on Mental Health kwakushirikiana
na Psychosocial Support in Emergency Settings (IASC MHPSS RG).
Yameandaa kitabu maalumu kwa ajili ya Watoto,wazazi,na walezi kwa kipindindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa wa corona( Covid-19) kuhakikisha watoto wana pata elimu ya kukabiliana na maambukizi ya Corona kwa usimamizi wa wazazi,walezi na waalimu wao.
Kitabu hiki kimeandaliwa kwa njia ya hadithi amabayo muhusika mkuu ni mtoto Sara akiwa na Mama yake mzazi anae muita SHUJAA WAKE kwa kushirikiana na watoto wenzake pamoja na watu wazima kuhusu kujikinga na maambukizi ya Covid-19.
Kitabu hiki kimepewa jina la “WEWE NDIO SHUJAA WANGU” Sisi pia Tanzania Kids Time tumeanza kukuwekea hadithi hii kwenye tovuti yetu jinsi watoto watakavyo chukua hatua ya kupambana dhidi ya corona maeneo waliopo.
Kitabu hiki kinakurasa 20 amba zimejaa maada zinazo wavutia watoto na kuwafundisha kwa njia ya picha na maandishi, hata hivyo TKT/UN RADIO tuta rekodi sauti kuatia hadithi nzima ilikuwezesha makundi yote kukielewa kitabu hiki kwa kushirikiana na wazazi,walezi na walimu wao, kwa mfano:Watoto Wenye uoni hafifu.