Wakati nchi ikiendeleza mapambano dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19, Viongozi wa Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro wamechukua hatua za ziada ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya hivyo kwa kuzuia mikusanyiko yoyote ya watoto katika mitaa.
Hayo yamezungumzwa na Afisa mtendaji wa Kata hiyo Bi, Hossana Kapinga katika mahojiano maalumu na TKT/UN RADIO kwa njia ya simu, ambapo wamewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto hunawa mikono, na kutoa taarifa kwa Viongozi wa mtaa endapo mgeni atafika nyumbani kutoka nje ya Mkoa huo.
“Wazazi waweze kuwanunulia watoto wao vitu vya kuchezea ili wakae nyumbani kuliko kuzurula ovyo mitaani, kuzecheza na watoto wengine na kuacha kuwagiza sokoni na madukani kwani kufanya hivyo watakuwa salama” amesema.
Aidha Afisa Afya wa Kata hiyo ya Bigwa Ramla Ramadhani amesema wamepiga marufuku kwenye mikusanyiko isio ya lazima vijiweni, kumbi za sinema ambazo watoto wengine hupenda kwenda na kuangalia michezo mbalimbali ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona(COVID 19)
Katika hatua nyinge ameeleza kuwa, Elimu wanayo isisitiza kwa mama mjamzito, ambaye ananyonyesha pamoja na watoto wadogo nikuhakikisha wanazingatia ulaji wa vyakula vyenye virutubisho bila kukosa matunda na mbogamboga kwani Kinga Ni Bora kuliko Tiba.
Baadhi ya wananchi akiwepo Raphael Mkaanga ambaye ni mkazi wa Bigwa amesema kuwa, wazazi na walezi wanapaswa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Viongozi wa serikali hususani lishe bora kwa watoto ili kuimalisha kinga mwilini dhidi ya magonjwa.
Awali Wizara ya Afya nchini ilieleza kuwa lishe nimuhimu kuzingatia kwani uwezo was mwali kupambana na maambukizi ya Covid-19 unategemea hali ya afya na lishe ya mtu.
Hivyo