Sehemu ya kwanza ya kitabu cha “WEWE NISHUJAA WANGU” kinacho husu watoto na Covid-19,kime wahusisha watoto na watu wazima na muhusika mkuu ni mtoto SARA na mama yake anaeitwa MUM.
Mama yake Sara ni shujaa wake kwa sababu yeye ndiye bora zaidi ulimwenguni.
SARA “COVID-19 inaonekanaje?” alimuuliza mama yake.
MUM“COVID-19 ! ni ndogo sana sisi
hatuwezi kuiona, “mama yakealimjibu.
“Lakini inaenea kupitia kikohozi,kupiga chafya kwa watu ambao ni wagonjwa,na kugusana kwa watu au vitu ambavyavyo vina virusi hivyo,Watu ambao ni wagonjwa hupata homa na kukohoa na utapata shida ya kupumuua “.
SARA “Kwani hatuwezi kupigana nayo?”aliuliza.
“Tunaweza kupigana,” alisema Mum”
Ndiyo maana nakuhitaji uwe salama, Sara. Kwani Virusi vime athiri watu wengi ulimwenguni, na kila mtu anaweza kumsaidia mwingine kwa kujikinga na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.
Watoto ni kundi maalum na wanaweza kua msaada pia kwa watoto wenzao na watu wazima,kwakuhakikisha hawachangamani na watu wengi,kunawa mikono kwa maji vugu vugu,dawa ya mikono na kukohoa kwa kufunika mdomo, pamoja na kuzingatia lishe kwa watoto.
“Wewe pia unahitaji kuwa shujaa wangu.”MUM alimwambia mtoto Sara.
SARA alilala kitandani usiku huo na alitaka kwenda shule lakini shule yake ilifungwa.
Alitaka kwenda kuwaona na kucheza na marafiki zake lakini hapakuwa salama.
SARA alitaka Virus vya corona kuuacha kuutisha ulimwengu nakuwatisha watoto wote na wazazi wao wote.
MUM ambae ni mama yake Sara alimwambia sara hata “wewe ni shujaa wangu” alitia moyo nakumwambia asilie na kuwa na hofu kila wakati kwani atacheza nyumbani,atasoma nyumbani na nibora kutii maelekezo ya wataalamu was afya ili kuwa salama na watoto wengine.
Wewe shujaa wako ninani?
Inaendelea kesho……