Ushiriki wa wananchi na Viongozi wa serikali za mitaa katika kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya homa Kali ya mapafu (Corona) mkoani Morogoro ni muhimu zaidi kwani utasaidia kupunguza maambukizi na kusambaa kwa Ugonjwa wa COVID19 nchini.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji wa kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro Bi. Jenipher Stephen katika mahojiano maalumu na Tkt/UN Radio, ambapo ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia ushauri wa Wataalamu Afya katika janga hili, licha ya kuwa hakuna maambukizi ya Corona katika kata hiyo.
Aidha Bi. Jenipher amebainisha mbinu wanayo tumia katika kata hiyo ili kuona Kama wananchi wanazingatia ushauri na maelekezo ya viongozi kwa kuzitembelea nyumba mbalimbali, ili kukagua uzingatiaji wa maji tiririka, vitakasa mikono pamoja na kufunga vituo vya masomo ya ziada kwa wanafunzi.
“Pamoja na hayo wazazi na Walezi wanapaswa kuingatia kuwapa lishe ya kutosha Watoto wakati huu ambapo wako nyumbani ili kuimalisha kinga za mwili, na kuendelea kuwafundisha Watoto namna ya kunawa mikono kwa maji tirika Safi na salama bila kusahau vitakasa mikono, lakini endapo mazazi analazimika kwenda mahali penye msongamano wa watu avae barakoa” alieleza.
Baadhi ya wananchi katika Kata ya Lukobe akiwepo Flowin Focus ameishukuru serikali kwa kusimamia na kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa COVID 19, huku akiwashauri wananchi kuacha kupuuza bali kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa Afya yanayotolewa juu ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa.
Naye Ester Jackson mkazi wa kata hiyo, ameiomba serikali kutoa elimu juu ya vyakula na Lishe Bora ambavyo inasaidia kuongeza Kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi hasa kwa Watoto na wajawazito.
Hii nzuri kabisa ni moja ya majukumu ya mzazi katika kumlinda mtoto dhidi ya korona. Watoto wengi hawajui kuchukia tahadhari ya ugonjwa huu hivyo wazazi waonbeze juhudi kuwafindisha namna ya kuchujua tahadhari ya Corona ikiwemo kunawa mikono. Hongera TKT.
Hii nzuri kabisa ni moja ya majukumu ya mzazi katika kumlinda mtoto dhidi ya corona. Watoto wengi hawajui kuchukia tahadhari ya ugonjwa huu hivyo wazazi waonbeze juhudi kuwafindisha namna ya kuchujua tahadhari ya Corona ikiwemo kunawa mikono. Hongera TKT.
Sure!! Wana-LUKOBE hatujaiangusha serikali kuu. Tumeitikia, ofisi ya kata kea pamoja na Baraza la Maendeleo Kata ya Lukobe tunaisimamia utekelezaji wa maelekezo yote ya kitaalam yanayoagizwa na mamlaka pia.