Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Mafiga, Manispaa ya Morogoro imewaandikia barua wenyeviti wa mitaa katika kata hiyo, ikiwataka kusimamia kikamilifu suala la uelimishaji wananchi pamoja na wazazi kuzuia Watoto wao kuzurula ovyo ili kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19.
Hayo yamebainishwa na Afisa mtendaji wa kata hiyo Asha Mvogogo wakati wa mahojiano maalumu na Tkt/ UN Radio kuhusu ushiriki wa wananchi na serikali katika Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona nchini.
Bi. Asha Mvogogo amesema kuwa, barua iliyoandikwa kwenda kwa wenyeviti wa mitaa ilikuwa na Lengo la kuwasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya kipindi hiki huku wakitakiwa kuweka maji tiririka na vitakasa mikono kwa kila nyumba pamoja na wazazi kuwa walinzi kwa Watoto.
“Wazazi na Walezi hakikisheni Watoto wenu hawazuruli ovyo mitaani pasipo na kazi za msingi, vinginevyo watoto watakaokutwa katika mikusanyiko isiyotakiwa watakamatwa na faini itatozwa kwa wazazi wao kwa kosa la kukiuka maagizo ya serikali”. Amesema
Kwa Upande wake Afisa Afya wa kata ya Mafiga Jackson Mwanga amesema kwamba, hadi sasa hakuna taarifa yeyote ya maambukizi ya mgojwa wa COVID19 katika kata hiyo, huku wakiendelea kutoa elimu ya namna ya kujikinga na Ugonjwa huo ikiwa Ni pamoja na kuzingatia Lishe hususani kwa watoto na mama wajawazito.
“kutokuwa na usafiri wa kutufikisha kila mtaa ili kuendelea kutoa elimu ya COVID19 kwa haraka, na kukagua maaeneo ya mtaa ni moja ya changamoto inayotukabiri viongozi, kwani elimu hiyo tunaitoa kwa kutembea kwa miguuu kuzunguka mitaa yote”. Ameeleza Mwanga
Hata hivyo Baadhi ya wakazi wa kata hiyo akiwepo Bi. Rehema Magembe amewaomba viongozi wa mtaa kuzungukia nyumba za wananchi kwani wapo ambao wanapuuzia agizo la serikali la unawaji mikono kwa maji Safi na vitakasa mikono.
” inashangaza kuona nyumba zenye wapangaji wengi hakuna maji tiririka Wala vitakasa mikono, watu wanatoka na kuingia bila ya kunawa tuache mazoea Ugonjwa huu Ni hatari, viongozi wapite kukagua waache kuangalia maeneo yenye biashara tu”. amesema.
Kazi nzuri sana TKT. Na maoni ya wenyeviti wa mtaa ni halisi kabisa kwani mtaani huko au majumbani huko hali si nziri kweli katika kuchukua tahadhari ya corono.
Kazi nzuri sana TKT. Na maoni ya wenyeviti wa mtaa ni halisi kabisa kwani mtaani huko au majumbani huko hali si nziri kweli katika kuchukua tahadhari ya corona.
Nikweli kabisa