Ofisi ya ustawi wa jamii mkoa wa Morogoro yatoa takwimu zake kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya watoto kwa mwaka 2018/2019 na January-March,Mwaka huu.
Akizungumza na Tkt/UN Radio hii leo kwa njia ya simu kwa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unao sababishwa na virusi vya Corona afisa ustawi wa jamii mkoa wa Morogoro Bi,Jesca Kagunila.
Kipindi cha mwaka 2018/2019 kesi zilizo wafikia jumla ni 1124 kwa mkoa mzima,
na kesi 349 zikafikishwa mahakamani huku kesi 36 zikitolewa hukumu.
Kesi zilizo ongoza kuripotiwa ni ukatili wa kingono,ambapo jumla kimkoa zilikuwa 513,kihisia 460 na kimwili 88.
Aidha bi,Kagunila amebainisha kwamba,wilaya ilio ongoza kwa kesi za matukio mengi kuripotiwa ni mji mdogo wa Ifakara matukio 316,Kilombero matukio 219,Hospital ya rufaa mkoa 213,Mvomero 131,Kilosa 104,Gairo 103,Ulanga92,Morogoro vijijini 91,Manspaa ya Morogoro 41 na wilaya ya Malinyi 27.
Wilaya zilizo ongoza kwa kesi za matukio ya mimba za utotoni ni:-
Ya kwanza ni Wilaya ya Kilosa kwa kuripotiwa kesi 932,Ulanga 194,Gairo118,Kilombero 89,Mvomero 44,Ifakara 35,Manispaa ya Morogoro 34,Morogoro vijijini 23.
Hata hivyo kesi za watoto walio kinzana na sheria ni 135 wote hawa wakiwa watoto wakiume,na watoto walio saidiwa kwa kupewa msaada mbali mbali kama vile chakula,maradhi,saikolojia na makazi ni 14294 kati ya hao 8100 ke, na 6195 me.
Kwa mwezi January- March mwaka huu jumla ya kesi za ukatili ulio ripotiwa ni 682 kwa mkoa mzima,kesi 56 zimefikishwa mahakamani na kesi 6 zimekwisha tolewa hukumu.
Ukatili ulio ongoza kwa robo hii ya kwanza ya mwaka huu wa 2020,ni ukatili wa kihisia ambapo hadi sasa ni kesi 253 zilizo ripotiwa,ukatili wa kingono kesi 166 na ukatili wa kimwili kesi 79.
Wilaya ulio ongoza kwa kesi za ukatili wa matukio mbali mbali ni:-
Ifakara zimeripotiwa kesi 478,Hospital ya rufaa kesi 72,Kilosa kesi 32,Mvomero kesi 30,Kilosa kesi 22,Manispaa kesi 17,Morogoro vijijini kesi 14,Ulanga kesi 8,Gairo kesi 8,Marinyi kesi 1.
Katika hautua nyingine bi,Kagunila amesema kwa mwaka huu wa 2020, kesi za mimba za utotoni jumla ni 239 na kesi za watoto walio kinzana na sheria ni 35 kwa mkoa mzima kufikia hivisasa,watoto walio saidiwa kupewa misaada mbali mbali kamavile,Lishe,kazi,elimu, na kisaikolojia jumla ni watoto 10178 ke,5015 na me,5063.
Bi,Jesca Kagunila akatoa wito kwa jamii,”Nawaomba wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuweni walinzi wa watoto, hata watoto msiogope kutoa taarifa kwenye vyombo husika.
Kuweni makini mjichunge kwa kipindi hiki cha ugonjwa wa covid-19,naleo nisiku ya maadhimisho ya mtoto wa afrika na watakia kumbukizi njema”mwisho wa kunukuu.