Mwenyekiti wa baraza la watoto Zanzibar Asiya Makame abainisha changamoto zilizopo visiwani humo kuhusu watoto.
“Swala la utumikishwaji kwa watoto huku Zanzibar bado lipo,asilimia kubwa nikwenye sekta ya uvuvi kwani watoto wanaenda kuvua na kuuza samaki”Amesema.
Aidha kwenye upande wakilimo, bi,Makame amesema” kwa baadhi ya wazazi na walezi wana wachukuwa watoto na kuwatumikisha kwenye mashamba,wakati huo hawaendi shule kwa baadhi ya maeneo kama vile eneo la Makunduchi.
Hata hivyo bi,Makame amewaomba wazazi na walezi, wahakikishe wanafahamu kilasiku watoto wao wanaenda shule kweli au la, kwani wengine wanaacha shule wanaenda kujifundisha English course ili wawe waongoza wageni wanao ingia visiwani humo.
Amebainisha hayo wakati wa mahojiano na TKT/UN RADIO kwa njia ya simu kuhusu siku ya Kupinga utumikishwaji kwa watoto ambayo huadhimishwa mwezi June ya kila mwaka.